Quran with Swahili translation - Surah Al-Fatihah ayat 6 - الفَاتِحة - Page - Juz 1
﴿ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ ﴾
[الفَاتِحة: 6]
﴿اهدنا الصراط المستقيم﴾ [الفَاتِحة: 6]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Tuonyeshe, tuongoze na tupe taufiki ya kuelekea njia iliyonyoka na ututhibitishe juu yake mpaka tukutane na wewe, nayo ni Uislamu ambao ndio njia iliyo wazi yenye kufikisha kwenye radhi za Mwenyezi Mungu na kwenye Pepo yake, njia tuliyoonyeshwa na aliye mwisho wa Mitume wa Mwenyezi Mungu na Manabii Wake, Muhammad, reheme ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwani hakuna kufaulu kwa mja isipokuwa kwa kusimama imara juu yake |