Quran with Swahili translation - Surah Al-Fatihah ayat 7 - الفَاتِحة - Page - Juz 1
﴿صِرَٰطَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِمۡ غَيۡرِ ٱلۡمَغۡضُوبِ عَلَيۡهِمۡ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ ﴾
[الفَاتِحة: 7]
﴿صراط الذين أنعمت عليهم غير المغضوب عليهم ولا الضالين﴾ [الفَاتِحة: 7]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Njia ya wale uliowaneemesha miongoni mwa Manabii, wakweli wa imani, mashahidi na wema. Wao ndio watu wa uongofu na kusimama imara. Na usitufanye kuwa miongoni mwa wale waliofuata njia ya waliokasirikiwa, wale walioijua haki na wasiifuate kivitendo, nao ni Mayahudi na wale waliofanana na wao; wala usitufanye ni miongoni mwa wapotevu, nao ni wale ambao hawakuongoka kwa ujinga waliokuwa nao, wakapotea njia, nao ni Wanaswara na waliofuata mwenendo wao. Katika dua hii kuna ponya ya moyo wa Muislamu ya ugonjwa wa ukanushaji, ujinga na upotevu, na ni dalili kwamba neema kubwa zaidi kuliko zote ni neema ya Uislamu. Basi mwenye kuwa mjuzi zaidi wa haki na akawa mfuataji zaidi wa hiyo haki, basi huwa ni aula zaidi wa njia iliyonyoka. Na hapana shaka kwamba Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ndio watu aula zaidi wa hilo baada ya Manabii, amani iwashukie. Basi aya hii yaonyesha utukufu wao na ukubwa wa daraja yao, Mwenyezi Mungu Awe radhi nao. Ni sunna kwa msomaji aseme katika Swala baada ya kusoma Fatiha «Āmīn», na maana yake ni: Ewe Mola! Takabali. Nayo si aya katika sura ya Fatiha kwa maafikiano ya wanavyuoni. Na kwa hivyo wamekubaliana kwa umoja wao kutoiandika kwenye Misahafu |