Quran with Swahili translation - Surah Al-Fatihah ayat 5 - الفَاتِحة - Page - Juz 1
﴿إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ ﴾
[الفَاتِحة: 5]
﴿إياك نعبد وإياك نستعين﴾ [الفَاتِحة: 5]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sisi tunakuabudu wewe peke yako, na tunataka msaada kwako peke yako katika mambo yetu yote. Mambo yote yako mkononi mwako, hakuna asiyekuwa wewe anayemiliki chochote katika hayo hata kadiri ya uzito wa chungu mdogo. Katika aya hii kuna dalili ya kuwa mja haifai aelekeze kitu chochote miongoni mwa aina za ibada, kama kuomba, kutaka kunusuriwa, kuchinja na kutufu, isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Pia ndani yake kuna ponya ya nyoyo kutokana na ugonjwa wa kufungamana na asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kutokana na ugonjwa wa ria, kujiona na kiburi |