Quran with Swahili translation - Surah An-Nazi‘at ayat 5 - النَّازعَات - Page - Juz 30
﴿فَٱلۡمُدَبِّرَٰتِ أَمۡرٗا ﴾
[النَّازعَات: 5]
﴿فالمدبرات أمرا﴾ [النَّازعَات: 5]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kwa Malaika wanaopitisha amri za Mola wao katika mambo ya ulimwengu waliowakilishwa kuyafanya na kuyasimamia, - Wala haifai kwa kiumbe kukiapia chochote kile, bali yapasa kiapo chake kiwe ni kwa jina la Mola wake Muumba au sifa Zake. Na lau ataapa kwa asiye Muumba wake, basi huyo amekuwa mshirikina - Watafufuliwa viumbe bila shaka na watahesabiwa |