وَالنَّازِعَاتِ غَرْقًا (1) Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu |
وَالنَّاشِطَاتِ نَشْطًا (2) Na kwa wanao toa kwa upole |
وَالسَّابِحَاتِ سَبْحًا (3) Na wanao ogelea |
فَالسَّابِقَاتِ سَبْقًا (4) Wakishindana mbio |
فَالْمُدَبِّرَاتِ أَمْرًا (5) Wakidabiri mambo |
يَوْمَ تَرْجُفُ الرَّاجِفَةُ (6) Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka |
تَتْبَعُهَا الرَّادِفَةُ (7) Kifuate cha kufuatia |
قُلُوبٌ يَوْمَئِذٍ وَاجِفَةٌ (8) Siku hiyo nyoyo zitapiga piga |
أَبْصَارُهَا خَاشِعَةٌ (9) Macho yatainama chini |
يَقُولُونَ أَإِنَّا لَمَرْدُودُونَ فِي الْحَافِرَةِ (10) Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza |
أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا نَّخِرَةً (11) Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa |
قَالُوا تِلْكَ إِذًا كَرَّةٌ خَاسِرَةٌ (12) Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara |
فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ (13) Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu |
فَإِذَا هُم بِالسَّاهِرَةِ (14) Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano |
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ (15) Je! Imekufikia hadithi ya Musa |
إِذْ نَادَاهُ رَبُّهُ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى (16) Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia |
اذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ (17) Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri |
فَقُلْ هَل لَّكَ إِلَىٰ أَن تَزَكَّىٰ (18) Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa |
وَأَهْدِيَكَ إِلَىٰ رَبِّكَ فَتَخْشَىٰ (19) Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha |
فَأَرَاهُ الْآيَةَ الْكُبْرَىٰ (20) Basi alimwonyesha Ishara kubwa |
فَكَذَّبَ وَعَصَىٰ (21) Lakini aliikadhibisha na akaasi |
ثُمَّ أَدْبَرَ يَسْعَىٰ (22) Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi |
فَحَشَرَ فَنَادَىٰ (23) Akakusanya watu akanadi |
فَقَالَ أَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ (24) Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa |
فَأَخَذَهُ اللَّهُ نَكَالَ الْآخِرَةِ وَالْأُولَىٰ (25) Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo |
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّمَن يَخْشَىٰ (26) Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa |
أَأَنتُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَمِ السَّمَاءُ ۚ بَنَاهَا (27) Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga |
رَفَعَ سَمْكَهَا فَسَوَّاهَا (28) Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri |
وَأَغْطَشَ لَيْلَهَا وَأَخْرَجَ ضُحَاهَا (29) Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake |
وَالْأَرْضَ بَعْدَ ذَٰلِكَ دَحَاهَا (30) Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi |
أَخْرَجَ مِنْهَا مَاءَهَا وَمَرْعَاهَا (31) Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake |
وَالْجِبَالَ أَرْسَاهَا (32) Na milima akaisimamisha |
مَتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ (33) Kwa nafuu yenu na mifugo yenu |
فَإِذَا جَاءَتِ الطَّامَّةُ الْكُبْرَىٰ (34) Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa |
يَوْمَ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ مَا سَعَىٰ (35) Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya |
وَبُرِّزَتِ الْجَحِيمُ لِمَن يَرَىٰ (36) Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona |
فَأَمَّا مَن طَغَىٰ (37) Basi ama yule aliye zidi ujeuri |
وَآثَرَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا (38) Na akakhiari maisha ya dunia |
فَإِنَّ الْجَحِيمَ هِيَ الْمَأْوَىٰ (39) Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake |
وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَىٰ (40) Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio |
فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَىٰ (41) Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake |
يَسْأَلُونَكَ عَنِ السَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَاهَا (42) Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini |
فِيمَ أَنتَ مِن ذِكْرَاهَا (43) Una nini wewe hata uitaje |
إِلَىٰ رَبِّكَ مُنتَهَاهَا (44) Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake |
إِنَّمَا أَنتَ مُنذِرُ مَن يَخْشَاهَا (45) Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu |
كَأَنَّهُمْ يَوْمَ يَرَوْنَهَا لَمْ يَلْبَثُوا إِلَّا عَشِيَّةً أَوْ ضُحَاهَا (46) Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake |