The Quran in Swahili - Surah Adiyat translated into Swahili, Surah Al-Adiyat in Swahili. We provide accurate translation of Surah Adiyat in Swahili - السواحيلية, Verses 11 - Surah Number 100 - Page 599.

| وَالْعَادِيَاتِ ضَبْحًا (1) Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua |
| فَالْمُورِيَاتِ قَدْحًا (2) Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini |
| فَالْمُغِيرَاتِ صُبْحًا (3) Wakishambulia wakati wa asubuhi |
| فَأَثَرْنَ بِهِ نَقْعًا (4) Huku wakitimua vumbi |
| فَوَسَطْنَ بِهِ جَمْعًا (5) Na wakijitoma kati ya kundi |
| إِنَّ الْإِنسَانَ لِرَبِّهِ لَكَنُودٌ (6) Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi |
| وَإِنَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌ (7) Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo |
| وَإِنَّهُ لِحُبِّ الْخَيْرِ لَشَدِيدٌ (8) Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali |
| ۞ أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِي الْقُبُورِ (9) Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini |
| وَحُصِّلَ مَا فِي الصُّدُورِ (10) Na yakakusanywa yaliomo vifuani |
| إِنَّ رَبَّهُم بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّخَبِيرٌ (11) Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote |