The Quran in Swahili - Surah Qariah translated into Swahili, Surah Al-Qariah in Swahili. We provide accurate translation of Surah Qariah in Swahili - السواحيلية, Verses 11 - Surah Number 101 - Page 600.

| الْقَارِعَةُ (1) Inayo gonga |
| مَا الْقَارِعَةُ (2) Nini Inayo gonga |
| وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْقَارِعَةُ (3) Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga |
| يَوْمَ يَكُونُ النَّاسُ كَالْفَرَاشِ الْمَبْثُوثِ (4) Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika |
| وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ الْمَنفُوشِ (5) Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa |
| فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ (6) Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito |
| فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ (7) Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza |
| وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ (8) Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu |
| فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ (9) Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya |
| وَمَا أَدْرَاكَ مَا هِيَهْ (10) Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo |
| نَارٌ حَامِيَةٌ (11) Ni Moto mkali |