القرآن باللغة السواحيلية - سورة العاديات مترجمة إلى اللغة السواحيلية، Surah Adiyat in Swahili. نوفر ترجمة دقيقة سورة العاديات باللغة السواحيلية - Swahili, الآيات 11 - رقم السورة 100 - الصفحة 599.
وَالْعَادِيَاتِ ضَبْحًا (1) Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua |
فَالْمُورِيَاتِ قَدْحًا (2) Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini |
فَالْمُغِيرَاتِ صُبْحًا (3) Wakishambulia wakati wa asubuhi |
فَأَثَرْنَ بِهِ نَقْعًا (4) Huku wakitimua vumbi |
فَوَسَطْنَ بِهِ جَمْعًا (5) Na wakijitoma kati ya kundi |
إِنَّ الْإِنسَانَ لِرَبِّهِ لَكَنُودٌ (6) Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi |
وَإِنَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌ (7) Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo |
وَإِنَّهُ لِحُبِّ الْخَيْرِ لَشَدِيدٌ (8) Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali |
۞ أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِي الْقُبُورِ (9) Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini |
وَحُصِّلَ مَا فِي الصُّدُورِ (10) Na yakakusanywa yaliomo vifuani |
إِنَّ رَبَّهُم بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّخَبِيرٌ (11) Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote |