The Quran in Swahili - Surah Ghashiya translated into Swahili, Surah Al-Ghashiyah in Swahili. We provide accurate translation of Surah Ghashiya in Swahili - السواحيلية, Verses 26 - Surah Number 88 - Page 592.
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ (1) Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza |
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ (2) Siku hiyo nyuso zitainama |
عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ (3) Zikifanya kazi, nazo taabani |
تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً (4) Ziingie katika Moto unao waka |
تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ آنِيَةٍ (5) Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka |
لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ (6) Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba |
لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِي مِن جُوعٍ (7) Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa |
وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ (8) Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu |
لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ (9) Zitakuwa radhi kwa juhudi yao |
فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ (10) Katika Bustani ya juu |
لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَاغِيَةً (11) Hawatasikia humo upuuzi |
فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ (12) Humo imo chemchem inayo miminika |
فِيهَا سُرُرٌ مَّرْفُوعَةٌ (13) Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa |
وَأَكْوَابٌ مَّوْضُوعَةٌ (14) Na bilauri zilizo pangwa |
وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ (15) Na matakia safu safu |
وَزَرَابِيُّ مَبْثُوثَةٌ (16) Na mazulia yaliyo tandikwa |
أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ (17) Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa |
وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ (18) Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa |
وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ (19) Na milima jinsi ilivyo thibitishwa |
وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ (20) Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa |
فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ (21) Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji |
لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ (22) Wewe si mwenye kuwatawalia |
إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ (23) Lakini anaye rudi nyuma na kukataa |
فَيُعَذِّبُهُ اللَّهُ الْعَذَابَ الْأَكْبَرَ (24) Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa |
إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ (25) Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao |
ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُم (26) Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao |