The Quran in Swahili - Surah Al Ala translated into Swahili, Surah Al-Ala in Swahili. We provide accurate translation of Surah Al Ala in Swahili - السواحيلية, Verses 19 - Surah Number 87 - Page 591.

| سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى (1) Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa |
| الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ (2) Aliye umba, na akaweka sawa |
| وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ (3) Na ambaye amekadiria na akaongoa |
| وَالَّذِي أَخْرَجَ الْمَرْعَىٰ (4) Na aliye otesha malisho |
| فَجَعَلَهُ غُثَاءً أَحْوَىٰ (5) Kisha akayafanya makavu, meusi |
| سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰ (6) Tutakusomesha wala hutasahau |
| إِلَّا مَا شَاءَ اللَّهُ ۚ إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ (7) Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana |
| وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ (8) Na tutakusahilishia yawe mepesi |
| فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ الذِّكْرَىٰ (9) Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa |
| سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ (10) Atakumbuka mwenye kuogopa |
| وَيَتَجَنَّبُهَا الْأَشْقَى (11) Na atajitenga mbali nayo mpotovu |
| الَّذِي يَصْلَى النَّارَ الْكُبْرَىٰ (12) Ambaye atauingia Moto mkubwa |
| ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ (13) Tena humo hatakufa wala hawi hai |
| قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ (14) Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa |
| وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّىٰ (15) Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali |
| بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا (16) Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia |
| وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ (17) Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi |
| إِنَّ هَٰذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ (18) Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo |
| صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ (19) Vitabu vya Ibrahimu na Musa |