×

Surah Al-Fajr in Swahili

Quran Swahili ⮕ Surah Fajr

Translation of the Meanings of Surah Fajr in Swahili - السواحيلية

The Quran in Swahili - Surah Fajr translated into Swahili, Surah Al-Fajr in Swahili. We provide accurate translation of Surah Fajr in Swahili - السواحيلية, Verses 30 - Surah Number 89 - Page 593.

بسم الله الرحمن الرحيم

وَالْفَجْرِ (1)
Naapa kwa alfajiri
وَلَيَالٍ عَشْرٍ (2)
Na kwa masiku kumi
وَالشَّفْعِ وَالْوَتْرِ (3)
Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja
وَاللَّيْلِ إِذَا يَسْرِ (4)
Na kwa usiku unapo pita
هَلْ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِي حِجْرٍ (5)
Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili
أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ (6)
Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di
إِرَمَ ذَاتِ الْعِمَادِ (7)
Wa Iram, wenye majumba marefu
الَّتِي لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِي الْبِلَادِ (8)
Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi
وَثَمُودَ الَّذِينَ جَابُوا الصَّخْرَ بِالْوَادِ (9)
Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni
وَفِرْعَوْنَ ذِي الْأَوْتَادِ (10)
Na Firauni mwenye vigingi
الَّذِينَ طَغَوْا فِي الْبِلَادِ (11)
Ambao walifanya jeuri katika nchi
فَأَكْثَرُوا فِيهَا الْفَسَادَ (12)
Wakakithirisha humo ufisadi
فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ (13)
Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu
إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ (14)
Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia
فَأَمَّا الْإِنسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ (15)
Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu
وَأَمَّا إِذَا مَا ابْتَلَاهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَهَانَنِ (16)
Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge
كَلَّا ۖ بَل لَّا تُكْرِمُونَ الْيَتِيمَ (17)
Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima
وَلَا تَحَاضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ (18)
Wala hamhimizani kulisha masikini
وَتَأْكُلُونَ التُّرَاثَ أَكْلًا لَّمًّا (19)
Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa
وَتُحِبُّونَ الْمَالَ حُبًّا جَمًّا (20)
Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi
كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا (21)
Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande
وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا (22)
Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu
وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَ ۚ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ وَأَنَّىٰ لَهُ الذِّكْرَىٰ (23)
Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini
يَقُولُ يَا لَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي (24)
Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu
فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ (25)
Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake
وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُ أَحَدٌ (26)
Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake
يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ (27)
Ewe nafsi iliyo tua
ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً (28)
Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha
فَادْخُلِي فِي عِبَادِي (29)
Basi ingia miongoni mwa waja wangu
وَادْخُلِي جَنَّتِي (30)
Na ingia katika Pepo yangu
❮ Previous Next ❯

Surahs from Quran :

1- Fatiha2- Baqarah
3- Al Imran4- Nisa
5- Maidah6- Anam
7- Araf8- Anfal
9- Tawbah10- Yunus
11- Hud12- Yusuf
13- Raad14- Ibrahim
15- Hijr16- Nahl
17- Al Isra18- Kahf
19- Maryam20- TaHa
21- Anbiya22- Hajj
23- Muminun24- An Nur
25- Furqan26- Shuara
27- Naml28- Qasas
29- Ankabut30- Rum
31- Luqman32- Sajdah
33- Ahzab34- Saba
35- Fatir36- Yasin
37- Assaaffat38- Sad
39- Zumar40- Ghafir
41- Fussilat42- shura
43- Zukhruf44- Ad Dukhaan
45- Jathiyah46- Ahqaf
47- Muhammad48- Al Fath
49- Hujurat50- Qaf
51- zariyat52- Tur
53- Najm54- Al Qamar
55- Rahman56- Waqiah
57- Hadid58- Mujadilah
59- Al Hashr60- Mumtahina
61- Saff62- Jumuah
63- Munafiqun64- Taghabun
65- Talaq66- Tahrim
67- Mulk68- Qalam
69- Al-Haqqah70- Maarij
71- Nuh72- Jinn
73- Muzammil74- Muddathir
75- Qiyamah76- Insan
77- Mursalat78- An Naba
79- Naziat80- Abasa
81- Takwir82- Infitar
83- Mutaffifin84- Inshiqaq
85- Buruj86- Tariq
87- Al Ala88- Ghashiya
89- Fajr90- Al Balad
91- Shams92- Lail
93- Duha94- Sharh
95- Tin96- Al Alaq
97- Qadr98- Bayyinah
99- Zalzalah100- Adiyat
101- Qariah102- Takathur
103- Al Asr104- Humazah
105- Al Fil106- Quraysh
107- Maun108- Kawthar
109- Kafirun110- Nasr
111- Masad112- Ikhlas
113- Falaq114- An Nas