القرآن باللغة السواحيلية - سورة الغاشية مترجمة إلى اللغة السواحيلية، Surah Ghashiya in Swahili. نوفر ترجمة دقيقة سورة الغاشية باللغة السواحيلية - Swahili, الآيات 26 - رقم السورة 88 - الصفحة 592.

| هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ (1) Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza |
| وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ (2) Siku hiyo nyuso zitainama |
| عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ (3) Zikifanya kazi, nazo taabani |
| تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً (4) Ziingie katika Moto unao waka |
| تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ آنِيَةٍ (5) Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka |
| لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ (6) Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba |
| لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِي مِن جُوعٍ (7) Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa |
| وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ (8) Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu |
| لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ (9) Zitakuwa radhi kwa juhudi yao |
| فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ (10) Katika Bustani ya juu |
| لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَاغِيَةً (11) Hawatasikia humo upuuzi |
| فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ (12) Humo imo chemchem inayo miminika |
| فِيهَا سُرُرٌ مَّرْفُوعَةٌ (13) Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa |
| وَأَكْوَابٌ مَّوْضُوعَةٌ (14) Na bilauri zilizo pangwa |
| وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ (15) Na matakia safu safu |
| وَزَرَابِيُّ مَبْثُوثَةٌ (16) Na mazulia yaliyo tandikwa |
| أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ (17) Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa |
| وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ (18) Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa |
| وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ (19) Na milima jinsi ilivyo thibitishwa |
| وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ (20) Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa |
| فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ (21) Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji |
| لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ (22) Wewe si mwenye kuwatawalia |
| إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ (23) Lakini anaye rudi nyuma na kukataa |
| فَيُعَذِّبُهُ اللَّهُ الْعَذَابَ الْأَكْبَرَ (24) Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa |
| إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ (25) Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao |
| ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُم (26) Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao |