The Quran in Swahili - Surah Lail translated into Swahili, Surah Al-Layl in Swahili. We provide accurate translation of Surah Lail in Swahili - السواحيلية, Verses 21 - Surah Number 92 - Page 595.

| وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ (1) Naapa kwa usiku unapo funika |
| وَالنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ (2) Na mchana unapo dhihiri |
| وَمَا خَلَقَ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ (3) Na kwa Aliye umba dume na jike |
| إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ (4) Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali |
| فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ (5) Ama mwenye kutoa na akamchamngu |
| وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ (6) Na akaliwafiki lilio jema |
| فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ (7) Tutamsahilishia yawe mepesi |
| وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ (8) Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake |
| وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ (9) Na akakanusha lilio jema |
| فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ (10) Tutamsahilishia yawe mazito |
| وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّىٰ (11) Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia |
| إِنَّ عَلَيْنَا لَلْهُدَىٰ (12) Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu |
| وَإِنَّ لَنَا لَلْآخِرَةَ وَالْأُولَىٰ (13) Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia |
| فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّىٰ (14) Basi nakuonyeni na Moto unao waka |
| لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى (15) Hatauingia ila mwovu kabisa |
| الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ (16) Anaye kadhibisha na kupa mgongo |
| وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى (17) Na mchamngu ataepushwa nao |
| الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّىٰ (18) Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa |
| وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰ (19) Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa |
| إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَىٰ (20) Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa |
| وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ (21) Naye atakuja ridhika |