القرآن باللغة السواحيلية - سورة الليل مترجمة إلى اللغة السواحيلية، Surah Lail in Swahili. نوفر ترجمة دقيقة سورة الليل باللغة السواحيلية - Swahili, الآيات 21 - رقم السورة 92 - الصفحة 595.
وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ (1) Naapa kwa usiku unapo funika |
وَالنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ (2) Na mchana unapo dhihiri |
وَمَا خَلَقَ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ (3) Na kwa Aliye umba dume na jike |
إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ (4) Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali |
فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ (5) Ama mwenye kutoa na akamchamngu |
وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ (6) Na akaliwafiki lilio jema |
فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ (7) Tutamsahilishia yawe mepesi |
وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ (8) Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake |
وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ (9) Na akakanusha lilio jema |
فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ (10) Tutamsahilishia yawe mazito |
وَمَا يُغْنِي عَنْهُ مَالُهُ إِذَا تَرَدَّىٰ (11) Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia |
إِنَّ عَلَيْنَا لَلْهُدَىٰ (12) Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu |
وَإِنَّ لَنَا لَلْآخِرَةَ وَالْأُولَىٰ (13) Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia |
فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّىٰ (14) Basi nakuonyeni na Moto unao waka |
لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى (15) Hatauingia ila mwovu kabisa |
الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ (16) Anaye kadhibisha na kupa mgongo |
وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى (17) Na mchamngu ataepushwa nao |
الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّىٰ (18) Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa |
وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰ (19) Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa |
إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَىٰ (20) Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa |
وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ (21) Naye atakuja ridhika |