The Quran in Swahili - Surah Duha translated into Swahili, Surah Ad-Dhuha in Swahili. We provide accurate translation of Surah Duha in Swahili - السواحيلية, Verses 11 - Surah Number 93 - Page 596.
وَالضُّحَىٰ (1) Naapa kwa mchana |
وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ (2) Na kwa usiku unapo tanda |
مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ (3) Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe |
وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ الْأُولَىٰ (4) Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia |
وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰ (5) Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike |
أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ (6) Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi |
وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَىٰ (7) Na akakukuta umepotea akakuongoa |
وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَىٰ (8) Akakukuta mhitaji akakutosheleza |
فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ (9) Basi yatima usimwonee |
وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ (10) Na anaye omba au kuuliza usimkaripie |
وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ (11) Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie |