وَالسَّمَاءِ وَالطَّارِقِ (1) Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku |
وَمَا أَدْرَاكَ مَا الطَّارِقُ (2) Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku |
النَّجْمُ الثَّاقِبُ (3) Ni Nyota yenye mwanga mkali |
إِن كُلُّ نَفْسٍ لَّمَّا عَلَيْهَا حَافِظٌ (4) Hapana nafsi ila inayo mwangalizi |
فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ مِمَّ خُلِقَ (5) Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani |
خُلِقَ مِن مَّاءٍ دَافِقٍ (6) Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa |
يَخْرُجُ مِن بَيْنِ الصُّلْبِ وَالتَّرَائِبِ (7) Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu |
إِنَّهُ عَلَىٰ رَجْعِهِ لَقَادِرٌ (8) Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha |
يَوْمَ تُبْلَى السَّرَائِرُ (9) Siku zitakapo dhihirishwa siri |
فَمَا لَهُ مِن قُوَّةٍ وَلَا نَاصِرٍ (10) Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi |
وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الرَّجْعِ (11) Naapa kwa mbingu yenye marejeo |
وَالْأَرْضِ ذَاتِ الصَّدْعِ (12) Na kwa ardhi inayo pasuka |
إِنَّهُ لَقَوْلٌ فَصْلٌ (13) Hakika hii ni kauli ya kupambanua |
وَمَا هُوَ بِالْهَزْلِ (14) Wala si mzaha |
إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًا (15) Hakika wao wanapanga mpango |
وَأَكِيدُ كَيْدًا (16) Na Mimi napanga mpango |
فَمَهِّلِ الْكَافِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًا (17) Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole |