The Quran in Swahili - Surah Al Balad translated into Swahili, Surah Al-Balad in Swahili. We provide accurate translation of Surah Al Balad in Swahili - السواحيلية, Verses 20 - Surah Number 90 - Page 594.
لَا أُقْسِمُ بِهَٰذَا الْبَلَدِ (1) Naapa kwa Mji huu |
وَأَنتَ حِلٌّ بِهَٰذَا الْبَلَدِ (2) Nawe unaukaa Mji huu |
وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ (3) Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa |
لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي كَبَدٍ (4) Hakika tumemuumba mtu katika taabu |
أَيَحْسَبُ أَن لَّن يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌ (5) Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza |
يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًا لُّبَدًا (6) Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali |
أَيَحْسَبُ أَن لَّمْ يَرَهُ أَحَدٌ (7) Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona |
أَلَمْ نَجْعَل لَّهُ عَيْنَيْنِ (8) Kwani hatukumpa macho mawili |
وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ (9) Na ulimi, na midomo miwili |
وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ (10) Na tukambainishia zote njia mbili |
فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ (11) Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani |
وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ (12) Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani |
فَكُّ رَقَبَةٍ (13) Kumkomboa mtumwa |
أَوْ إِطْعَامٌ فِي يَوْمٍ ذِي مَسْغَبَةٍ (14) Au kumlisha siku ya njaa |
يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ (15) Yatima aliye jamaa |
أَوْ مِسْكِينًا ذَا مَتْرَبَةٍ (16) Au masikini aliye vumbini |
ثُمَّ كَانَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا بِالْمَرْحَمَةِ (17) Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana |
أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ (18) Hao ndio watu wa kheri wa kuliani |
وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا هُمْ أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ (19) Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni |
عَلَيْهِمْ نَارٌ مُّؤْصَدَةٌ (20) Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande |