القرآن باللغة السواحيلية - سورة البلد مترجمة إلى اللغة السواحيلية، Surah Al Balad in Swahili. نوفر ترجمة دقيقة سورة البلد باللغة السواحيلية - Swahili, الآيات 20 - رقم السورة 90 - الصفحة 594.

| لَا أُقْسِمُ بِهَٰذَا الْبَلَدِ (1) Naapa kwa Mji huu | 
| وَأَنتَ حِلٌّ بِهَٰذَا الْبَلَدِ (2) Nawe unaukaa Mji huu | 
| وَوَالِدٍ وَمَا وَلَدَ (3) Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa | 
| لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ فِي كَبَدٍ (4) Hakika tumemuumba mtu katika taabu | 
| أَيَحْسَبُ أَن لَّن يَقْدِرَ عَلَيْهِ أَحَدٌ (5) Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza | 
| يَقُولُ أَهْلَكْتُ مَالًا لُّبَدًا (6) Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali | 
| أَيَحْسَبُ أَن لَّمْ يَرَهُ أَحَدٌ (7) Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona | 
| أَلَمْ نَجْعَل لَّهُ عَيْنَيْنِ (8) Kwani hatukumpa macho mawili | 
| وَلِسَانًا وَشَفَتَيْنِ (9) Na ulimi, na midomo miwili | 
| وَهَدَيْنَاهُ النَّجْدَيْنِ (10) Na tukambainishia zote njia mbili | 
| فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ (11) Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani | 
| وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ (12) Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani | 
| فَكُّ رَقَبَةٍ (13) Kumkomboa mtumwa | 
| أَوْ إِطْعَامٌ فِي يَوْمٍ ذِي مَسْغَبَةٍ (14) Au kumlisha siku ya njaa | 
| يَتِيمًا ذَا مَقْرَبَةٍ (15) Yatima aliye jamaa | 
| أَوْ مِسْكِينًا ذَا مَتْرَبَةٍ (16) Au masikini aliye vumbini | 
| ثُمَّ كَانَ مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ وَتَوَاصَوْا بِالْمَرْحَمَةِ (17) Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana | 
| أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ الْمَيْمَنَةِ (18) Hao ndio watu wa kheri wa kuliani | 
| وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا هُمْ أَصْحَابُ الْمَشْأَمَةِ (19) Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni | 
| عَلَيْهِمْ نَارٌ مُّؤْصَدَةٌ (20) Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande |