Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 177 - البَقَرَة - Page - Juz 2
﴿۞ لَّيۡسَ ٱلۡبِرَّ أَن تُوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ قِبَلَ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ وَلَٰكِنَّ ٱلۡبِرَّ مَنۡ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةِ وَٱلۡكِتَٰبِ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ وَءَاتَى ٱلۡمَالَ عَلَىٰ حُبِّهِۦ ذَوِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينَ وَٱبۡنَ ٱلسَّبِيلِ وَٱلسَّآئِلِينَ وَفِي ٱلرِّقَابِ وَأَقَامَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَى ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلۡمُوفُونَ بِعَهۡدِهِمۡ إِذَا عَٰهَدُواْۖ وَٱلصَّٰبِرِينَ فِي ٱلۡبَأۡسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ وَحِينَ ٱلۡبَأۡسِۗ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ صَدَقُواْۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُتَّقُونَ ﴾
[البَقَرَة: 177]
﴿ليس البر أن تولوا وجوهكم قبل المشرق والمغرب ولكن البر من آمن﴾ [البَقَرَة: 177]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hapana kheri, mbele ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, kuelekea kwenye Swala upande wa mashariki na magharibi, iwapo hilo halitokamani na amri ya Mwenyezi Mungu na sheria Yake. Hakika kheri yote iko katika imani ya aliyemuamini Mwenyezi Mungu na akamkubali kuwa Ndiye muabudiwa, Peke Yake, Hana mshirika Wake, na akaiamini Siku ya kufufuliwa na Malipo, na akawaamini Malaika wote na vitabu vyote vilivyoteremshwa, na Mitume wote bila kubagua, na akatoa mali yake kwa hiyari yake, pamoja na kuwa anayapenda sana, kuwapa jamaa zake na mayatima wenye uhitaji waliofiliwa na wazazi wao hali wao wako chini ya umri wa kubaleghe, na akawapa masikini ambao ufukara umewaelemea, na wasafiri wanaohitaji walio mbali na watu wao na mali yao, na waombaji ambao imekuwa ni dharura kwao kuomba kwa uhitaji wao mkubwa, na akatoa mali yake katika kuwakomboa watumwa na mateka, na akasimamisha Swala na akatoa zaka za faradhi, na wale wenye kutekeleza ahadi, na mwenye kusubiri katika hali ya ufukara wake na ugonjwa wake na katika vita vikali. Hao wenye kusifika kwa sifa hizo, ndio waliokuwa wakweli katika imani zao, na wao ndio waliojikinga mateso ya Mwenyezi Mungu wakajiepusha na vitendo vya kumuasi |