×

Enyi mlio amini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katika walio uwawa - muungwana 2:178 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:178) ayat 178 in Swahili

2:178 Surah Al-Baqarah ayat 178 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 178 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡقِصَاصُ فِي ٱلۡقَتۡلَىۖ ٱلۡحُرُّ بِٱلۡحُرِّ وَٱلۡعَبۡدُ بِٱلۡعَبۡدِ وَٱلۡأُنثَىٰ بِٱلۡأُنثَىٰۚ فَمَنۡ عُفِيَ لَهُۥ مِنۡ أَخِيهِ شَيۡءٞ فَٱتِّبَاعُۢ بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَأَدَآءٌ إِلَيۡهِ بِإِحۡسَٰنٖۗ ذَٰلِكَ تَخۡفِيفٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَرَحۡمَةٞۗ فَمَنِ ٱعۡتَدَىٰ بَعۡدَ ذَٰلِكَ فَلَهُۥ عَذَابٌ أَلِيمٞ ﴾
[البَقَرَة: 178]

Enyi mlio amini! Mmepewa ruhusa kulipa kisasi katika walio uwawa - muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, na mwanamke kwa mwanamke. Na anaye samehewa na ndugu yake chochote basi ashikwe kulipa kwa wema, na yeye alipe kwa ihsani. Huko ni kupunguziwa kuliko tokana na Mola wenu Mlezi, na ni rehema. Na atakaye vuka mipaka baada ya haya, basi yeye atapata adhabu chungu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ياأيها الذين آمنوا كتب عليكم القصاص في القتلى الحر بالحر والعبد بالعبد, باللغة السواحيلية

﴿ياأيها الذين آمنوا كتب عليكم القصاص في القتلى الحر بالحر والعبد بالعبد﴾ [البَقَرَة: 178]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafanya vitendo vinavyoambatana na Sheria ya Mwenyezi Mungu Alioifanya faradhi kwenu kwamba mlipize kisasi kwa muuaji aliyeua kwa kukusudia, kwa sharti ya kufanya usawa na kufananisha malipo: auawe muungwana kwa kumuua mfano wake, na mtumwa kwa mfano wake, na mwanamke kwa mfano wake. Na yule atakayesamehewa na msimamizi wa aliyeuawa kwa kumuondolea kisasi na kutosheka kwa kuchukua dia, nayo ni kiwango cha mali maalumu akitoacho mhalifu kikiwa ni badali ya kusamehewa, ni juu ya pande mbili zijilazimishe tabia njema: yule msimamizi adai diya yake bila kutumia nguvu, na yule muuaji ampatiye haki yake kwa wema bila kuchelewesha wala kupunguza. Msamaha huo, pamoja na kupokea hiyo dia, ni masahilisho ya Mola wenu na ni huruma kwenu kwa ule usahali na kujinufaisha. Hivyo basi,mwenye kumuua muuaji baada ya msamaha na kupokea dia, atapata adhabu kali ya kuuawa kwa njia ya kisasi duniani au kutiwa Motoni Akhera
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek