×

Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani 2:275 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:275) ayat 275 in Swahili

2:275 Surah Al-Baqarah ayat 275 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 275 - البَقَرَة - Page - Juz 3

﴿ٱلَّذِينَ يَأۡكُلُونَ ٱلرِّبَوٰاْ لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ ٱلَّذِي يَتَخَبَّطُهُ ٱلشَّيۡطَٰنُ مِنَ ٱلۡمَسِّۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡبَيۡعُ مِثۡلُ ٱلرِّبَوٰاْۗ وَأَحَلَّ ٱللَّهُ ٱلۡبَيۡعَ وَحَرَّمَ ٱلرِّبَوٰاْۚ فَمَن جَآءَهُۥ مَوۡعِظَةٞ مِّن رَّبِّهِۦ فَٱنتَهَىٰ فَلَهُۥ مَا سَلَفَ وَأَمۡرُهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِۖ وَمَنۡ عَادَ فَأُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ ﴾
[البَقَرَة: 275]

Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet'ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: الذين يأكلون الربا لا يقومون إلا كما يقوم الذي يتخبطه الشيطان من, باللغة السواحيلية

﴿الذين يأكلون الربا لا يقومون إلا كما يقوم الذي يتخبطه الشيطان من﴾ [البَقَرَة: 275]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Wale wenye kuamiliana kwa riba- nayo ni nyongeza juu ya rasilmali-, hawainuki kutoka kwenye makaburi yao Siku ya Mwisho isipokuwa ni kama anavyoinuka yule anayepigwa na Shetani akapatwa na wazimu. Hivo ni kwa kuwa wao walisema kwamba biashara ni kama riba, kwa kuwa yote mawili ni halali na yanapelekea mali kuongezeka. Mwenyezi Mungu Akawakanusha na Akabainisha kwamba Yeye Amehalalisha biashara na Ameharamisha riba. Kwa kuwa katika kuuza na kununua kuna nafuu kwa watu binafsi na kwa jamii na katika riba kuna unyonyaji, hasara na maangamivu. Basi mwenye kumfikia yeye makatazo ya Mwenyezi Mungu ya riba akakomeka, achukue iliyopita kabla ya kumfikia yeye uharamu wake, na hana makosa kwa hilo. Na mambo yake ya siku zake za baadae yako kwa Mwenyezi Mungu. Akiwa ataendelea na toba yake, basi Mwenyezi Mungu Hapotezi malipo ya wenye kufanya wema; na akiwa atarudia kwenye riba, basi kitendo chake hiko baada ya kufikiwa na makatazo ya Mwenyezi Mungu, kitamfanya astahili mateso, kwa kuwa hoja imesimama juu yake. Kwa ajili ya hii Alisema Mwenyezi Mungu, «Basi hao ni watu wa Motoni; Wao ndani yake watakaa milele»
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek