×

Kisha nyinyi kwa nyinyi mnauwana, na mnawatoa baadhi yenu majumbani kwao, mkisaidiana 2:85 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:85) ayat 85 in Swahili

2:85 Surah Al-Baqarah ayat 85 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 85 - البَقَرَة - Page - Juz 1

﴿ثُمَّ أَنتُمۡ هَٰٓؤُلَآءِ تَقۡتُلُونَ أَنفُسَكُمۡ وَتُخۡرِجُونَ فَرِيقٗا مِّنكُم مِّن دِيَٰرِهِمۡ تَظَٰهَرُونَ عَلَيۡهِم بِٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡعُدۡوَٰنِ وَإِن يَأۡتُوكُمۡ أُسَٰرَىٰ تُفَٰدُوهُمۡ وَهُوَ مُحَرَّمٌ عَلَيۡكُمۡ إِخۡرَاجُهُمۡۚ أَفَتُؤۡمِنُونَ بِبَعۡضِ ٱلۡكِتَٰبِ وَتَكۡفُرُونَ بِبَعۡضٖۚ فَمَا جَزَآءُ مَن يَفۡعَلُ ذَٰلِكَ مِنكُمۡ إِلَّا خِزۡيٞ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يُرَدُّونَ إِلَىٰٓ أَشَدِّ ٱلۡعَذَابِۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ ﴾
[البَقَرَة: 85]

Kisha nyinyi kwa nyinyi mnauwana, na mnawatoa baadhi yenu majumbani kwao, mkisaidiana kwa dhambi na uadui. Na wakikujieni mateka mnawakomboa, na hali kuwatoa mmekatazwa. Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakataa baadhi yake? Basi hana malipo mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayo yatenda

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ثم أنتم هؤلاء تقتلون أنفسكم وتخرجون فريقا منكم من ديارهم تظاهرون عليهم, باللغة السواحيلية

﴿ثم أنتم هؤلاء تقتلون أنفسكم وتخرجون فريقا منكم من ديارهم تظاهرون عليهم﴾ [البَقَرَة: 85]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kisha nyinyi kwa nyinyi mnauana, baadhi yenu wanawaua wengine, na baadhi yenu wanawatoa wengine majumbani mwao; na kila kundi kati yenu linajitafutia nguvu kwa maadui dhidi ya ndugu zake kwa njia ya udhalimu na uonevu. Na mkijiwa nao, hao ndugu zenu, ni mateka kwenye mikono ya maadui, mnafanya haraka kuwakomboa kwa kulipa fidia, pamoja na kuwa imeharamishwa kwenu kuwatoa majumbani mwao. Ni ubaya ulioje mnaoufanya wa kuziamini baadhi ya hukumu za Taurati na kuzikanusha nyingine! Basi Malipo ya wanaoyafanaya hayo si mengine ila ni unyonge na fedheha ulimwenguni, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali sana ndani ya Moto. Na Mwenyezi Mungu si Mwenye kughafilika kwa mnayoyafanya
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek