Quran with Swahili translation - Surah Al-Qasas ayat 32 - القَصَص - Page - Juz 20
﴿ٱسۡلُكۡ يَدَكَ فِي جَيۡبِكَ تَخۡرُجۡ بَيۡضَآءَ مِنۡ غَيۡرِ سُوٓءٖ وَٱضۡمُمۡ إِلَيۡكَ جَنَاحَكَ مِنَ ٱلرَّهۡبِۖ فَذَٰنِكَ بُرۡهَٰنَانِ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦٓۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ ﴾
[القَصَص: 32]
﴿اسلك يدك في جيبك تخرج بيضاء من غير سوء واضمم إليك جناحك﴾ [القَصَص: 32]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Tia mkono wako kwenye uwazi wa kanzu yako uliofunguliwa kifuani na uutoe, utatoka kuwa mweupe, kama barafu, ambao si wa ugonjwa wala mbalanga, na ujikumbatie kwa mikono yako ili usalimike na kicho. Hivi viwili nilivyokuonesha, ewe Mūsā, vya fimbo kugeuka nyoka na kuufanya mkono wako kuwa mweupe na wenye kung’ara, si kwa ugonjwa wala mbalanga, ni dalili mbili kutoka kwa Mola wako, uende nazo kwa Fir’awn na watukufu wa watu wake.» Hakika Fir’awn na viongozi walio karibu naye walikuwa ni wakanushaji |