×

Na Musa akawateuwa watu sabiini katika kaumu yake kwa miadi yetu. Na 7:155 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:155) ayat 155 in Swahili

7:155 Surah Al-A‘raf ayat 155 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 155 - الأعرَاف - Page - Juz 9

﴿وَٱخۡتَارَ مُوسَىٰ قَوۡمَهُۥ سَبۡعِينَ رَجُلٗا لِّمِيقَٰتِنَاۖ فَلَمَّآ أَخَذَتۡهُمُ ٱلرَّجۡفَةُ قَالَ رَبِّ لَوۡ شِئۡتَ أَهۡلَكۡتَهُم مِّن قَبۡلُ وَإِيَّٰيَۖ أَتُهۡلِكُنَا بِمَا فَعَلَ ٱلسُّفَهَآءُ مِنَّآۖ إِنۡ هِيَ إِلَّا فِتۡنَتُكَ تُضِلُّ بِهَا مَن تَشَآءُ وَتَهۡدِي مَن تَشَآءُۖ أَنتَ وَلِيُّنَا فَٱغۡفِرۡ لَنَا وَٱرۡحَمۡنَاۖ وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلۡغَٰفِرِينَ ﴾
[الأعرَاف: 155]

Na Musa akawateuwa watu sabiini katika kaumu yake kwa miadi yetu. Na ulipo fika mtetemeko mkubwa alisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ungeli taka ungeli wahiliki wao na mimi zamani! Unatuhiliki kwa waliyo yafanya wajinga katika sisi? Haya si chochote ila ni mtihani wako, umpoteze umtakaye na umhidi umtakaye. Wewe ndiye Rafiki Mlinzi wetu. Basi tughufirie na uturehemu. Na Wewe ndiye mbora wa kughufiria

❮ Previous Next ❯

ترجمة: واختار موسى قومه سبعين رجلا لميقاتنا فلما أخذتهم الرجفة قال رب لو, باللغة السواحيلية

﴿واختار موسى قومه سبعين رجلا لميقاتنا فلما أخذتهم الرجفة قال رب لو﴾ [الأعرَاف: 155]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na Mūsā alichagua miongoni mwa watu wake wanaume sabiini walio bora kati yao, akatoka na wao akaenda hadi Tū,r Sīnā’ kwa wakati na muda ambao Mwenyezi Mungu Alimuagizia akutane na Yeye pamoja nao ili watubie kwa yale yaliyokuwa kwa wahuni wa Wana wa Isrāīl ya kuabudu kigombe. Walipokuja mahala hapo walisema, «Hatutakuamini, ewe Mūsā mpaka tumuone Mwenyezi Mungu waziwazi, basi utakaposema na Yeye tuoneshe.» Papo hapo walishikwa na mtetemeko mkali wakafa. Akasimama Mūsā akimnyenyekea Mwenyezi Mungu na akasema, «Ewe Mola wangu, niwaambie nini Wana wa Isrāīl nikiwajia na hali wewe umewaangamiza wabora wao? Lau unataka ungaliwaangamiza wote kabla ya hali hii ya kuwa mimi niko na wao. Hilo lingalikuwa sahali zaidi kwangu. Unatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wachache wa akili miongoni mwetu? Kitendo hiki ambacho watu wangu wamekifanya cha kuabudu kigombe, hakikuwa isipokuwa ni majaribu na mtihani, unampoteza kwayo unayemtaka miongoni mwa viumbe wako na unamuongoza kwayo unayemtaka kumuongoza. Ni wewe mtegemewa wetu na mwenye kutunusuru, tughufirie dhambi zetu na uturehemu kwa rehema zako; na wewe ndiye bora wa wenye kusamehe makosa na kusitiri dhambi
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek