Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 93 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿۞ إِنَّمَا ٱلسَّبِيلُ عَلَى ٱلَّذِينَ يَسۡتَـٔۡذِنُونَكَ وَهُمۡ أَغۡنِيَآءُۚ رَضُواْ بِأَن يَكُونُواْ مَعَ ٱلۡخَوَالِفِ وَطَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ ﴾
[التوبَة: 93]
﴿إنما السبيل على الذين يستأذنونك وهم أغنياء رضوا بأن يكونوا مع الخوالف﴾ [التوبَة: 93]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika makosa na lawama ni kwa wale matajiri waliokujia, ewe Mutme, kukutaka ruhusa ya kujikalia, nao ni wanafiki matajiri waliojichagulia kuketi pamoja na wanawake na wenye nyudhuru. Na Mwenyezi Mungu Amezipiga mhuri nyoyo zao kwa unafiki, haziingiwi na Imani. Wao hawajui mwisho wao mbaya kwa kubakia kwao nyuma na kuacha kwao kupigana jihadi pamoja na wewe |