Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 94 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿يَعۡتَذِرُونَ إِلَيۡكُمۡ إِذَا رَجَعۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡۚ قُل لَّا تَعۡتَذِرُواْ لَن نُّؤۡمِنَ لَكُمۡ قَدۡ نَبَّأَنَا ٱللَّهُ مِنۡ أَخۡبَارِكُمۡۚ وَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمۡ وَرَسُولُهُۥ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ﴾
[التوبَة: 94]
﴿يعتذرون إليكم إذا رجعتم إليهم قل لا تعتذروا لن نؤمن لكم قد﴾ [التوبَة: 94]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Watataka udhuru kwenu, enyi Wumini, hawa waliojikalisha nyuma na kuacha kupigana jihadi na washirikina, kwa kutumia maneno ya urongo, mtakaporudi kutoka kwenye jihadi ya vita vya Tabūk. Waambie, ewe Mtume, «Msitoe udhuru, hatutawaamini katika yale mnayoyasema. Mwenyezi Mungu Ashatupa habari, kuhusu mambo yenu, ambazo zimetupa uthibitisho wa urongo wenu. Mwenyezi Mungu Atayaona matendo yenu na Mtume Wake, iwapo mtatubia unafiki wenu au mtaendelea nao. Na Mwenyezi Mungu Atawaonesha watu matendo yenu waziwazi hapa duniani kisha mtarudishwa, baada ya kufa kwenu, kwa Yule Ambaye hayafichiki Kwake mambo yenu ya ndani na ya nje, ili Awape habari ya matendo yenu yote na Awape malipo yake |