The Quran in Swahili - Surah Al Alaq translated into Swahili, Surah Al-Alaq in Swahili. We provide accurate translation of Surah Al Alaq in Swahili - السواحيلية, Verses 19 - Surah Number 96 - Page 597.

| اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ (1) Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba |
| خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ (2) Amemuumba binaadamu kwa tone la damu |
| اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ (3) Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote |
| الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ (4) Ambaye amefundisha kwa kalamu |
| عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ (5) Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui |
| كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ (6) Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri |
| أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ (7) Akijiona katajirika |
| إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ (8) Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo |
| أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ (9) Umemwona yule anaye mkataza |
| عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ (10) Mja anapo sali |
| أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ (11) Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu |
| أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ (12) Au anaamrisha uchamngu |
| أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ (13) Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma |
| أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّهَ يَرَىٰ (14) Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona |
| كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ (15) Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele |
| نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ (16) Shungi la uwongo, lenye makosa |
| فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ (17) Basi na awaite wenzake |
| سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ (18) Nasi tutawaita Mazabania |
| كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ۩ (19) Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee |