القرآن باللغة السواحيلية - سورة العلق مترجمة إلى اللغة السواحيلية، Surah Al Alaq in Swahili. نوفر ترجمة دقيقة سورة العلق باللغة السواحيلية - Swahili, الآيات 19 - رقم السورة 96 - الصفحة 597.
اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ (1) Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba |
خَلَقَ الْإِنسَانَ مِنْ عَلَقٍ (2) Amemuumba binaadamu kwa tone la damu |
اقْرَأْ وَرَبُّكَ الْأَكْرَمُ (3) Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote |
الَّذِي عَلَّمَ بِالْقَلَمِ (4) Ambaye amefundisha kwa kalamu |
عَلَّمَ الْإِنسَانَ مَا لَمْ يَعْلَمْ (5) Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui |
كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ (6) Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri |
أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ (7) Akijiona katajirika |
إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ (8) Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo |
أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ (9) Umemwona yule anaye mkataza |
عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ (10) Mja anapo sali |
أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ (11) Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu |
أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ (12) Au anaamrisha uchamngu |
أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ (13) Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma |
أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّهَ يَرَىٰ (14) Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona |
كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ (15) Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele |
نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ (16) Shungi la uwongo, lenye makosa |
فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ (17) Basi na awaite wenzake |
سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ (18) Nasi tutawaita Mazabania |
كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ۩ (19) Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee |