Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 21 - يُوسُف - Page - Juz 12
﴿وَقَالَ ٱلَّذِي ٱشۡتَرَىٰهُ مِن مِّصۡرَ لِٱمۡرَأَتِهِۦٓ أَكۡرِمِي مَثۡوَىٰهُ عَسَىٰٓ أَن يَنفَعَنَآ أَوۡ نَتَّخِذَهُۥ وَلَدٗاۚ وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلِنُعَلِّمَهُۥ مِن تَأۡوِيلِ ٱلۡأَحَادِيثِۚ وَٱللَّهُ غَالِبٌ عَلَىٰٓ أَمۡرِهِۦ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ ﴾
[يُوسُف: 21]
﴿وقال الذي اشتراه من مصر لامرأته أكرمي مثواه عسى أن ينفعنا أو﴾ [يُوسُف: 21]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wasafiri walipoondoka na Yūsuf kuelekea Misri, kiongozi wake alimnunua, naye ni waziri, na akamwambia mke wake, «Kaa naye vizuri na uyafanye mema makazi yake kwetu, huenda tukafaidika na utumishi wake, au tukamuweka hapa kwetu kama mtoto.» Na kama tulivyomuokoa Yūsuf na tukamfanaya kiongozi wa Misri kuwa na huruma na yeye, vilevile tulimmakinisha kwenye ardhi ya Misri na tulimfanya asimamie hazina zake, na ili tumfundishe kuagua ndoto na apate kujua kwa uaguze huo matukio ya wakati unaokuja. Na Mwenyezi Mungu ni Mshindi kwa jambo Lake, uamuzi Wake ni wenye kupita, hakuna Mwenye kuutangua, lakini wengi sana kati ya watu hawajui kwamba mambo yote yako kwenye mkono wa Mwenyezi Mungu |