Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 67 - يُوسُف - Page - Juz 13
﴿وَقَالَ يَٰبَنِيَّ لَا تَدۡخُلُواْ مِنۢ بَابٖ وَٰحِدٖ وَٱدۡخُلُواْ مِنۡ أَبۡوَٰبٖ مُّتَفَرِّقَةٖۖ وَمَآ أُغۡنِي عَنكُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٍۖ إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِۖ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُۖ وَعَلَيۡهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُتَوَكِّلُونَ ﴾
[يُوسُف: 67]
﴿وقال يابني لا تدخلوا من باب واحد وادخلوا من أبواب متفرقة وما﴾ [يُوسُف: 67]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na akasema baba Yao kuwaambia wao,»Enyi wanangu mtakapoingia nchi ya Misri, msiingie kwa mlango mmoja, lakini ingieni kwa milango mbalimbali, ili msipatwe na jicho la husuda. Na mimi nikiwapa wasia huu, siwakingi na chochote Alichokiamua Mwenyezi Mungu kwenu. Hakuna uwamuzi wowote isipokuwa ni ule wa Mwenyezi Mungu Peke Yake, Kwake Yeye nimetegemea na nimeamini, na juu Yake Peke Yake waumini wanategemea.» |