Quran with Swahili translation - Surah Al-Isra’ ayat 71 - الإسرَاء - Page - Juz 15
﴿يَوۡمَ نَدۡعُواْ كُلَّ أُنَاسِۭ بِإِمَٰمِهِمۡۖ فَمَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَقۡرَءُونَ كِتَٰبَهُمۡ وَلَا يُظۡلَمُونَ فَتِيلٗا ﴾
[الإسرَاء: 71]
﴿يوم ندعوا كل أناس بإمامهم فمن أوتي كتابه بيمينه فأولئك يقرءون كتابهم﴾ [الإسرَاء: 71]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbuka, ewe Mtume, Siku ya Kufufuliwa, kwa njia ya kutoa bishara na kuogopesha, pindi Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na ktukuka, Atakapoliita kila kundi la watu pamoja na kiongozi wao ambaye walikuwa wakimfuata ulimwenguni. Basi aliyekuwa mwema kati yao , na akapewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, hawa watasoma kitabu cha mema yao wakiwa katika hali ya kufurahika na kuterema, na kamwe hawatapunguziwa chochote katika malipo ya matendo yao mazuri, hata kama ni kadiri ya uzi unaokuwa kwenye mpasuko wa koko ya tende |