×

Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na 2:102 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:102) ayat 102 in Swahili

2:102 Surah Al-Baqarah ayat 102 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 102 - البَقَرَة - Page - Juz 1

﴿وَٱتَّبَعُواْ مَا تَتۡلُواْ ٱلشَّيَٰطِينُ عَلَىٰ مُلۡكِ سُلَيۡمَٰنَۖ وَمَا كَفَرَ سُلَيۡمَٰنُ وَلَٰكِنَّ ٱلشَّيَٰطِينَ كَفَرُواْ يُعَلِّمُونَ ٱلنَّاسَ ٱلسِّحۡرَ وَمَآ أُنزِلَ عَلَى ٱلۡمَلَكَيۡنِ بِبَابِلَ هَٰرُوتَ وَمَٰرُوتَۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنۡ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَآ إِنَّمَا نَحۡنُ فِتۡنَةٞ فَلَا تَكۡفُرۡۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنۡهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِۦ بَيۡنَ ٱلۡمَرۡءِ وَزَوۡجِهِۦۚ وَمَا هُم بِضَآرِّينَ بِهِۦ مِنۡ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمۡ وَلَا يَنفَعُهُمۡۚ وَلَقَدۡ عَلِمُواْ لَمَنِ ٱشۡتَرَىٰهُ مَا لَهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ مِنۡ خَلَٰقٖۚ وَلَبِئۡسَ مَا شَرَوۡاْ بِهِۦٓ أَنفُسَهُمۡۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ ﴾
[البَقَرَة: 102]

Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua

❮ Previous Next ❯

ترجمة: واتبعوا ما تتلوا الشياطين على ملك سليمان وما كفر سليمان ولكن الشياطين, باللغة السواحيلية

﴿واتبعوا ما تتلوا الشياطين على ملك سليمان وما كفر سليمان ولكن الشياطين﴾ [البَقَرَة: 102]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na Mayahudi walifuata yale ambayo mashetani walikuwa wanawasimulia wachawi katika kipindi cha ufalme wa Sulaimān mwana wa Dāwūd. Na Sulaymān hakukufuru na wala hakujifundisha uchawi. Lakini mashetani ndio walimkanusha Mwenyezi Mungu kwa kuwafundisha watu uchawi, kwa kuwaharibia dini yao. Mayahudi pia waliufuata uchawi ulioshushwa kwa malaika wawili: Hārūt na Mārūt, katika ardhi ya Babil ilyoko Iraq, ukiwa ni mtihani na majaribio kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja Wake. Na hao Malaika wawili hawakuwa wakimfunza yoyote mpaka wamnasihi na kumuonya asijifunze uchawi na kumwambia, “Usikufuru kwa kujifunza uchawi na kuwatii mashetani.” Basi watu walikuwa wakijifunza kutoka kwa Malaika wawili vitu vinavyozusha chuki baina ya mume na mke mpaka wakafarikana. Na wachawi hawana uwezo wa kumdhuru, kwa uchawi wao, yoyote isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na hukumu Yake. Na wachawi hawajifunzi ila shari yenye kuwadhuru na kutowapa nafuu. Mashetani waliupeleka uchawi kwa Mayahudi, ukaenea kwao mpaka wakaufadhilisha juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Na Mayahudi walijua kwamba mwenye kuchagua uchawi na kuacha haki, hatakuwa na fungu lolote la kheri huko Akhera. Ni ubaya ulioje uchawi na ukafiri waliojichagulia nafsi zao kuwa ni badala ya Imani na kumfuata Mtume, lau walikuwa na elimu yenye kuzalisha vitendo vya kufuata mawaidha wapewayo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek