×

Hakika vilima vya Safaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu. 2:158 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Baqarah ⮕ (2:158) ayat 158 in Swahili

2:158 Surah Al-Baqarah ayat 158 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 158 - البَقَرَة - Page - Juz 2

﴿۞ إِنَّ ٱلصَّفَا وَٱلۡمَرۡوَةَ مِن شَعَآئِرِ ٱللَّهِۖ فَمَنۡ حَجَّ ٱلۡبَيۡتَ أَوِ ٱعۡتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَاۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيۡرٗا فَإِنَّ ٱللَّهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ ﴾
[البَقَرَة: 158]

Hakika vilima vya Safaa na Marwa ni katika alama za Mwenyezi Mungu. Basi anaye hiji kwenye Nyumba hiyo au akafanya Umra, si kosa kwake kuvizunguka. Na anaye jitendea mwenyewe kheri basi bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani na Mjuzi

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إن الصفا والمروة من شعائر الله فمن حج البيت أو اعتمر فلا, باللغة السواحيلية

﴿إن الصفا والمروة من شعائر الله فمن حج البيت أو اعتمر فلا﴾ [البَقَرَة: 158]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hakika Swafa na Marwa, nayo ni majabali mawili madogo karibu ya Alkaba upande wa Mashariki, ni miongoni mwa alama za dini ya Mwenyezi Mungu zilizo wazi ambazo Mwenyezi Mungu Amezifanya ni sehemu za ibada kwa waja Wake kusai baina yake. Hivyo basi, yoyote mwenye kuikusudia Alkaba kwa kuhiji au kufanya Umra, si dhambi kwake kusai baina ya hayo majabali mawili, bali ni wajibu kwake kufanya hivyo. Na yule mwenye kufanya mambo ya kutii amri, kwa hiyari yake, hali ya kumtakasia Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushukuru, Analipa juu ya kichache kwa kingi, ni Mwenye kuzijua amali za waja Wake: Hazipotezi wala Hampunji yoyote chochote hata kama ni uzito wa chungu mdogo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek