Quran with Swahili translation - Surah Al-Baqarah ayat 273 - البَقَرَة - Page - Juz 3
﴿لِلۡفُقَرَآءِ ٱلَّذِينَ أُحۡصِرُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ لَا يَسۡتَطِيعُونَ ضَرۡبٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ يَحۡسَبُهُمُ ٱلۡجَاهِلُ أَغۡنِيَآءَ مِنَ ٱلتَّعَفُّفِ تَعۡرِفُهُم بِسِيمَٰهُمۡ لَا يَسۡـَٔلُونَ ٱلنَّاسَ إِلۡحَافٗاۗ وَمَا تُنفِقُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٌ ﴾
[البَقَرَة: 273]
﴿للفقراء الذين أحصروا في سبيل الله لا يستطيعون ضربا في الأرض يحسبهم﴾ [البَقَرَة: 273]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wapeni sadaka zenu mafukara Waislamu ambao hawawezi kusafiri kutafuta riziki, kwa kuwa wameshughulika na jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, ambao huwadhania wao wasiowajua kuwa hawahitaji sadaka kwa kuwa wamejizuia na kuomba.Utawajua kwa alama zao na athari ya uhitaji walionao. Hawaombi kabisa. Na wakiomba, kwa kukosa budi, hawaombi kwa utiriri. Na mali yoyote mnayoyatoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, hakuna chochote, katika hayo, chenye kufichika kwa Mwenyezi Mungu.Na Mwenyezi Mungu Atalipa kwayo malipo mengi zaidi na makamilifu zaidi Siku ya Kiyama |