Quran with Swahili translation - Surah Ar-Rum ayat 50 - الرُّوم - Page - Juz 21
﴿فَٱنظُرۡ إِلَىٰٓ ءَاثَٰرِ رَحۡمَتِ ٱللَّهِ كَيۡفَ يُحۡيِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَآۚ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ ﴾
[الرُّوم: 50]
﴿فانظر إلى آثار رحمة الله كيف يحي الأرض بعد موتها إن ذلك﴾ [الرُّوم: 50]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Basi Tazama, ewe mwenye kuangalia, mtazamo wa kutia akilini na kuzingatia, athari za mvua kwenye mimea, nafaka na miti, ujionee vipi Mwenyezi Mungu Anaipa uhai ardhi baada ya kuwa imekufa, Akaiotesha mimea na nyasi? Hakika Yule aliyeweza kuihuisha ardhi hii Ndiye Atakayehuisha wafu, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza, hakuna kinachomshinda |