Quran with Swahili translation - Surah FaTir ayat 32 - فَاطِر - Page - Juz 22
﴿ثُمَّ أَوۡرَثۡنَا ٱلۡكِتَٰبَ ٱلَّذِينَ ٱصۡطَفَيۡنَا مِنۡ عِبَادِنَاۖ فَمِنۡهُمۡ ظَالِمٞ لِّنَفۡسِهِۦ وَمِنۡهُم مُّقۡتَصِدٞ وَمِنۡهُمۡ سَابِقُۢ بِٱلۡخَيۡرَٰتِ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَضۡلُ ٱلۡكَبِيرُ ﴾
[فَاطِر: 32]
﴿ثم أورثنا الكتاب الذين اصطفينا من عبادنا فمنهم ظالم لنفسه ومنهم مقتصد﴾ [فَاطِر: 32]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kisha tukawapa Qur’ani, baada ya ummah waliopita kuangamia, wale tuliowachagua miongoni mwa umati wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie: kati yao kuna aliyeidhulumu nafsi yake kwa kufanya baadhi ya maasia, na kati yao kuna aliyekuwa wastani, naye ni yule mwenye kutekeleza yaliyo wajibu na kuepuka yaliyoharamishwa, na katika wao kuna mwenye kutangulia kufanya mambo ya kheri kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, yaani mwenye kukimbilia na kujitahidi kufanya amali njema, za faradhi na za ziada. Na kupewa Kitabu huko na kuchaguliwa ummah huu ndio nyongeza kubwa |