×

Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua 39:23 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Az-Zumar ⮕ (39:23) ayat 23 in Swahili

39:23 Surah Az-Zumar ayat 23 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Az-Zumar ayat 23 - الزُّمَر - Page - Juz 23

﴿ٱللَّهُ نَزَّلَ أَحۡسَنَ ٱلۡحَدِيثِ كِتَٰبٗا مُّتَشَٰبِهٗا مَّثَانِيَ تَقۡشَعِرُّ مِنۡهُ جُلُودُ ٱلَّذِينَ يَخۡشَوۡنَ رَبَّهُمۡ ثُمَّ تَلِينُ جُلُودُهُمۡ وَقُلُوبُهُمۡ إِلَىٰ ذِكۡرِ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ هُدَى ٱللَّهِ يَهۡدِي بِهِۦ مَن يَشَآءُۚ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنۡ هَادٍ ﴾
[الزُّمَر: 23]

Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za wenye kumkhofu Mola wao Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoa amtakaye. Na ambaye ameachwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hapana wa kumwongoa

❮ Previous Next ❯

ترجمة: الله نـزل أحسن الحديث كتابا متشابها مثاني تقشعر منه جلود الذين يخشون, باللغة السواحيلية

﴿الله نـزل أحسن الحديث كتابا متشابها مثاني تقشعر منه جلود الذين يخشون﴾ [الزُّمَر: 23]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Aliteremsha Mazungumzo mazuri zaidi kuliko yote, nayo ni Qur’ani tukufu, inayofanana katika uzuri wake, upangikaji wake na kutotafautiana kwake, ndani yake mna hadithi, hukumu, hoja na dalili zilizo wazi. Kusomwa kwake kunarudiwa na ule wingi wa kuikariri hauifanyi ichokeshe. Isomwapo huifanya miili ya wenye kuisikia itetemeke na zitikisike ngozi za wale wanaomuogopa Mola wao, kwa kuathirika na yale yaliyomo ndani yake ya kutisha na kuonya, kisha zikalainika ngozi zao na nyoyo zao kwa kufurahia bishara iliyomo ya ahadi njema na mahimizo ya kufanya kheri. Kuathirika huko na Qur’ani ni uongofu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja Wake. Na yoyote yule ambaye Mwenyezi Mungu Anayempoteza asiiamini hii Qur’ani kwa sababu ya ukafiri wake na ushindani wake, basi hana muongozi mwenye kumuongoa na kumuafikia
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek