Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 13 - النِّسَاء - Page - Juz 4
﴿تِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۚ وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ يُدۡخِلۡهُ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ ﴾
[النِّسَاء: 13]
﴿تلك حدود الله ومن يطع الله ورسوله يدخله جنات تجري من تحتها﴾ [النِّسَاء: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hukumu hizo za Kimungu zilizowekwa na Mwenyezi Mungu, kuhusu mayatima, wanawake na mirathi, ni Sheria Zake zioneshazo kuwa zinatoka kwa Mwenyezi Mungu Aliye Mjuzi, Aliye Mwingi wa hekima. Na yoyote mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika hukumu hizi na nyenginezo zilizowekwa na Mwenyezi Mungu kwa waja Wake, Atamuingiza kwenye mabustani ya Peponi, yenye miti mingi na majumba ya fahari mengi, inayopita chini yake mito yenye maji tamu. Watasalia kwenye neema hii, hawatoki humo. Malipo hayo ndio kufuzu kukubwa |