×

Na wawili kati yenu wafanyao hayo waadhibuni. Na wakitubia wakatengenea basi waacheni. 4:16 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah An-Nisa’ ⮕ (4:16) ayat 16 in Swahili

4:16 Surah An-Nisa’ ayat 16 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah An-Nisa’ ayat 16 - النِّسَاء - Page - Juz 4

﴿وَٱلَّذَانِ يَأۡتِيَٰنِهَا مِنكُمۡ فَـَٔاذُوهُمَاۖ فَإِن تَابَا وَأَصۡلَحَا فَأَعۡرِضُواْ عَنۡهُمَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ تَوَّابٗا رَّحِيمًا ﴾
[النِّسَاء: 16]

Na wawili kati yenu wafanyao hayo waadhibuni. Na wakitubia wakatengenea basi waacheni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba, Mwenye kurehemu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: واللذان يأتيانها منكم فآذوهما فإن تابا وأصلحا فأعرضوا عنهما إن الله كان, باللغة السواحيلية

﴿واللذان يأتيانها منكم فآذوهما فإن تابا وأصلحا فأعرضوا عنهما إن الله كان﴾ [النِّسَاء: 16]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na wawili wenye kujiingiza kwenye kitendo cha uzinifu basi waudhini kwa kuwapiga, kuwahama na kuwaaibisha. Wakitubia na kitendo walichokifanya na wakajirekebisha kwa kufanya mambo mema, wasameheni na kuacha kuwaudhi. Faida inayotokana na aya hii na ile kabla yake ni kwamba wanaume wakifanya kitendo cha uzinifu wataudhiwa., ama wanawake watafungwa na kuudhiwa. Kifungo, kikomo chake ni kifo. Na udhia, kikomo chake ni toba na kutengea. Hii ilikuwako mwanzo wa Uislamu, kisha ikaondolewa kwa Sheria iliowekwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, nayo ni kupigwa mawe mpaka kufa, kwa yule ambaye ashaoa au ashaolewa, wakiwa wote wawili ni watu huru, waliobaleghe, wenye akili na ambao wameingilia au kuingiliwa katika ndoa sahihi. Ama wasiokuwa hao, adhabu yao ni kupigwa mbati mia na kuhamishwa mwaka mzima. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzikubali toba za waja Wake wanaotubia, ni Mwenye huruma kwao
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek