Quran with Swahili translation - Surah Al-Ma’idah ayat 70 - المَائدة - Page - Juz 6
﴿لَقَدۡ أَخَذۡنَا مِيثَٰقَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَأَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡهِمۡ رُسُلٗاۖ كُلَّمَا جَآءَهُمۡ رَسُولُۢ بِمَا لَا تَهۡوَىٰٓ أَنفُسُهُمۡ فَرِيقٗا كَذَّبُواْ وَفَرِيقٗا يَقۡتُلُونَ ﴾
[المَائدة: 70]
﴿لقد أخذنا ميثاق بني إسرائيل وأرسلنا إليهم رسلا كلما جاءهم رسول بما﴾ [المَائدة: 70]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwa hakika tulichukuwa ahadi ya mkazo kwa Wana wa Isrāīl katika Taurati kuwa watasikia na watatii na tukawapelekea kwa ahadi hiyo Mitume wetu. Lakini walivunja ile ahadi iliyochukuliwa kwao, wakafuata matamanio yao na wakawa kila akiwajia Mtume, miongoni mwa hao Mitume, kwa yale ambayo nafsi zao haziyataki, wanamfanyia uadui: wakawakanusha baadhi yao na wakawaua wengine |