×

Amekuumbieni namna nane za wanyama: Wawili katika kondoo, na wawili katika mbuzi. 6:143 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:143) ayat 143 in Swahili

6:143 Surah Al-An‘am ayat 143 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 143 - الأنعَام - Page - Juz 8

﴿ثَمَٰنِيَةَ أَزۡوَٰجٖۖ مِّنَ ٱلضَّأۡنِ ٱثۡنَيۡنِ وَمِنَ ٱلۡمَعۡزِ ٱثۡنَيۡنِۗ قُلۡ ءَآلذَّكَرَيۡنِ حَرَّمَ أَمِ ٱلۡأُنثَيَيۡنِ أَمَّا ٱشۡتَمَلَتۡ عَلَيۡهِ أَرۡحَامُ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۖ نَبِّـُٔونِي بِعِلۡمٍ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ﴾
[الأنعَام: 143]

Amekuumbieni namna nane za wanyama: Wawili katika kondoo, na wawili katika mbuzi. Sema je, ameharimisha yote madume wawili au majike wawili, au waliomo matumboni mwa majike yote mawili? Niambieni kwa ilimu ikiwa nyinyi mnasema kweli

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ثمانية أزواج من الضأن اثنين ومن المعز اثنين قل آلذكرين حرم أم, باللغة السواحيلية

﴿ثمانية أزواج من الضأن اثنين ومن المعز اثنين قل آلذكرين حرم أم﴾ [الأنعَام: 143]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Wanyama hawa ambao Mwenyezi Mungu Amewaruzuku waja Wake, miongoni mwa ngamia, ng’ombe, mbuzi na kondoo, ni aina nane: nne kati ya hizo ni mbuzi na kondoo, nao ni kondoo: waume na wake, na mbuzi: wume na wake. Sema, ewe Mtume, uwaambie hao washirikina, «Kwani Mwenyezi Mungu Amewaharamisha madume wawili wa mbuzi na kondoo?» Wakisema, «Ndio», watakuwa wamesema urongo kuhusu hilo. Sababu wao hawalifanyi kila dume la kondoo na mbuzi kuwa ni haramu. Na waambie, «Kwani Mwenyezi Mungu Amewaharamisha majike wawili wa mbuzi na kondoo?» wakisema, «Ndio», watakuwa pia wamesema urongo. Sababu wao hawamuharamishi kila mwanambuzi na mwanakondoo mke. Na sema uwaambie, «Kwani Mwenyezi Mungu Amewaharamisha watoto walio matumboni mwa majike wawili wa mbuzi na kondoo walio na mimba?» Wakisema, «Ndio.» Watakuwa wamesema urongo pia. Kwani hawaiharamishi kila mimba ya namna hiyo. Nambieni kwa misingi ya elimu inayoonesha usahihi wa msimamo wenu, mkiwa ni wakweli katika hayo mnayoyanasibisha kwa Mola wenu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek