Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 176 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَلَوۡ شِئۡنَا لَرَفَعۡنَٰهُ بِهَا وَلَٰكِنَّهُۥٓ أَخۡلَدَ إِلَى ٱلۡأَرۡضِ وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُۚ فَمَثَلُهُۥ كَمَثَلِ ٱلۡكَلۡبِ إِن تَحۡمِلۡ عَلَيۡهِ يَلۡهَثۡ أَوۡ تَتۡرُكۡهُ يَلۡهَثۚ ذَّٰلِكَ مَثَلُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۚ فَٱقۡصُصِ ٱلۡقَصَصَ لَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ ﴾
[الأعرَاف: 176]
﴿ولو شئنا لرفعناه بها ولكنه أخلد إلى الأرض واتبع هواه فمثله كمثل﴾ [الأعرَاف: 176]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau tulitaka kukitukuza cheo chake kwa aya tulizompa tungalifanya, lakini yeye alitegemea ulimwengu na akafuata matamanio yake, na akafadhilisha ladha zake na hawaa zake juu ya Akhera, na akakataa kumtii Mwenyezi Mungu na akaenda kinyume na amri Yake. Mfano wa mwanamume huyu ni mfano wa mbwa: ukimfukuza au ukimuacha hutoa ulimi wake katika hali zote mbili. Basi hivyo ndivyo alivyo yule aliyejivua aya za Mwenyezi Mungu kwa kuziacha, huwa akiendelea katika ukafiri wake ikiwa utafanya bidii kumlingania au utampuuza. Sifa hii, ewe Mtume, ndiyo sifa ya watu hawa waliokuwa wapotevu kabla hujawajia kwa uongofu na utume. Basi simulia, ewe Mtume, habari za watu waliopita, kwani katika kutolea kwako habari zao ni miujiza mikubwa zaidi; na huenda watu wako wakazingatia juu ya yale uliyowajia nayo na wakakuamini |