Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 67 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتُ بَعۡضُهُم مِّنۢ بَعۡضٖۚ يَأۡمُرُونَ بِٱلۡمُنكَرِ وَيَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَقۡبِضُونَ أَيۡدِيَهُمۡۚ نَسُواْ ٱللَّهَ فَنَسِيَهُمۡۚ إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ ﴾
[التوبَة: 67]
﴿المنافقون والمنافقات بعضهم من بعض يأمرون بالمنكر وينهون عن المعروف ويقبضون أيديهم﴾ [التوبَة: 67]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike ni aina moja katika kutangaza kwao Imani na kuficha kwao ukafiri. Wanaamrisha kukufuriwa Mwenyezi Mungu na kuasiwa Mtume Wake, na wanakataza Imani na utiifu, na wanaizuia mikono yao kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu. Wamemsahau Mwenyezi Mungu na kwa hivyo hawamtaji, na Yeye Amewasahau na rehema Yake hakuwaelekeza kwenye wema. Hakika wanafiki ndio waliotoka nje wakaacha kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake |