Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 68 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتِ وَٱلۡكُفَّارَ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ هِيَ حَسۡبُهُمۡۚ وَلَعَنَهُمُ ٱللَّهُۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ مُّقِيمٞ ﴾
[التوبَة: 68]
﴿وعد الله المنافقين والمنافقات والكفار نار جهنم خالدين فيها هي حسبهم ولعنهم﴾ [التوبَة: 68]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Amewaahidi wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike na Makafiri kwamba mwisho wao ni kwenda kwenye Moto wa Jahanamu, wakae humo milele kabisa. Moto huo ni wenye kuwatosha, ukiwa ni mateso yao kwa kumkanusha kwao Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu Amewafukuza kwenye rehema Yake. Na watakua na adhabu ya daima |