Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 8 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿كَيۡفَ وَإِن يَظۡهَرُواْ عَلَيۡكُمۡ لَا يَرۡقُبُواْ فِيكُمۡ إِلّٗا وَلَا ذِمَّةٗۚ يُرۡضُونَكُم بِأَفۡوَٰهِهِمۡ وَتَأۡبَىٰ قُلُوبُهُمۡ وَأَكۡثَرُهُمۡ فَٰسِقُونَ ﴾
[التوبَة: 8]
﴿كيف وإن يظهروا عليكم لا يرقبوا فيكم إلا ولا ذمة يرضونكم بأفواههم﴾ [التوبَة: 8]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Tabia ya Makafiri ni kujilazimisha na makubaliano iwapo ushindi uko kwa wengine wasiokuwa wao. Lakini wakijihisi kuwa wana nguvu juu ya Waumini, basi wao hawachungi ujamaa wala makubaliano. Basi msidanganyike na vile wanavyowafanyia wawapo na kicho na nyinyi. Kwani wao wanawaambia maneno kwa ndimi zao ili mridhike na wao, lakini nyoyo zao zinakataa hilo. Na wengi wao ni wenye kuupiga vita Uislamu, ni wenye kuvunja ahadi |