القرآن باللغة السواحيلية - سورة الأعلى مترجمة إلى اللغة السواحيلية، Surah Al Ala in Swahili. نوفر ترجمة دقيقة سورة الأعلى باللغة السواحيلية - Swahili, الآيات 19 - رقم السورة 87 - الصفحة 591.
سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى (1) Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa |
الَّذِي خَلَقَ فَسَوَّىٰ (2) Aliye umba, na akaweka sawa |
وَالَّذِي قَدَّرَ فَهَدَىٰ (3) Na ambaye amekadiria na akaongoa |
وَالَّذِي أَخْرَجَ الْمَرْعَىٰ (4) Na aliye otesha malisho |
فَجَعَلَهُ غُثَاءً أَحْوَىٰ (5) Kisha akayafanya makavu, meusi |
سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰ (6) Tutakusomesha wala hutasahau |
إِلَّا مَا شَاءَ اللَّهُ ۚ إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ (7) Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana |
وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ (8) Na tutakusahilishia yawe mepesi |
فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ الذِّكْرَىٰ (9) Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa |
سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ (10) Atakumbuka mwenye kuogopa |
وَيَتَجَنَّبُهَا الْأَشْقَى (11) Na atajitenga mbali nayo mpotovu |
الَّذِي يَصْلَى النَّارَ الْكُبْرَىٰ (12) Ambaye atauingia Moto mkubwa |
ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ (13) Tena humo hatakufa wala hawi hai |
قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ (14) Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa |
وَذَكَرَ اسْمَ رَبِّهِ فَصَلَّىٰ (15) Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali |
بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا (16) Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia |
وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ (17) Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi |
إِنَّ هَٰذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ (18) Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo |
صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ (19) Vitabu vya Ibrahimu na Musa |