Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 3 - يُونس - Page - Juz 11
﴿إِنَّ رَبَّكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ إِذۡنِهِۦۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡ فَٱعۡبُدُوهُۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ﴾
[يُونس: 3]
﴿إن ربكم الله الذي خلق السموات والأرض في ستة أيام ثم استوى﴾ [يُونس: 3]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika Mola wenu ni Mwenyezi Mungu Ambaye Alizipatisha mbingu na ardhi katika kipindi cha Siku Sita, kisha Akalingana, yaani Akawa juu ya 'Arsh, mlingano unaonasibiana na utisho Wake na utukufu Wake. Anaendesha mambo ya viumbe Vyake. Hakuna yoyote Anayempinga katika uamuzi Wake na hakuna muombezi yoyote anayeombea mbele Yake Siku ya Kiyama isipokuwa baada ya Yeye kumpa idhini kuombea. Basi muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wenu, Anayesifika kwa sifa hizi na mtakasiyeni ibada. Je, hamwaidhiki na mkazizingatia aya hizi na hoja |