×

Kwake Yeye tu ndio marejeo yenu nyote. Hii ni ahadi ya Mwenyezi 10:4 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Yunus ⮕ (10:4) ayat 4 in Swahili

10:4 Surah Yunus ayat 4 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 4 - يُونس - Page - Juz 11

﴿إِلَيۡهِ مَرۡجِعُكُمۡ جَمِيعٗاۖ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقًّاۚ إِنَّهُۥ يَبۡدَؤُاْ ٱلۡخَلۡقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ لِيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ بِٱلۡقِسۡطِۚ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَهُمۡ شَرَابٞ مِّنۡ حَمِيمٖ وَعَذَابٌ أَلِيمُۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡفُرُونَ ﴾
[يُونس: 4]

Kwake Yeye tu ndio marejeo yenu nyote. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli. Hakika Yeye ndiye aliye anzisha uumbaji, na kisha ataurejesha ili awalipe kwa uadilifu wale walio amini na wakatenda mema. Na walio kufuru, wao watapata vinywaji vinavyo chemka, na adhabu chungu kwa sababu ya walivyo kuwa wakikufuru

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إليه مرجعكم جميعا وعد الله حقا إنه يبدأ الخلق ثم يعيده ليجزي, باللغة السواحيلية

﴿إليه مرجعكم جميعا وعد الله حقا إنه يبدأ الخلق ثم يعيده ليجزي﴾ [يُونس: 4]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Kwa Mola wenu ndio marejeo yenu nyote Siku ya Kiyama. Na hili ndilo agizo la Mwenyezi Mungu lililo kweli. Yeye Ndiye Ambaye Anaanza kuumba viumbe kisha Atawarudisha baada ya kufa, Awafanye wawe hai kama walivyokuwa mwanzo, ili Awalipe waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na akafanya matendo mazuri malipo mazuri zaidi kwa uadilifu. Na wale waliokanusha upweke wa Mwenyezi Mungu na ujumbe wa Mtume Wake watakuwa na vinywaji vya maji moto sana yanayochoma nyuso na kukata tumbo; na watakuwa na adhabu inayoumiza kwa sababu ya ukafiri wao na upotevu wao
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek