Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 88 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَقَالَ مُوسَىٰ رَبَّنَآ إِنَّكَ ءَاتَيۡتَ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَأَهُۥ زِينَةٗ وَأَمۡوَٰلٗا فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا رَبَّنَا لِيُضِلُّواْ عَن سَبِيلِكَۖ رَبَّنَا ٱطۡمِسۡ عَلَىٰٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ وَٱشۡدُدۡ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَلَا يُؤۡمِنُواْ حَتَّىٰ يَرَوُاْ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَلِيمَ ﴾
[يُونس: 88]
﴿وقال موسى ربنا إنك آتيت فرعون وملأه زينة وأموالا في الحياة الدنيا﴾ [يُونس: 88]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mūsā akasema, «Mola wetu, hakika wewe umempa Fir'awn na watukufu wa watu wake pambo la vitu vya duniani wasikushukuru, na wamejisaidia kwa vitu hivyo katika kupotoa watu na njia Yako. Mola wetu, yageuze Mali yao wasifaidike nayo, na uzipige mhuri nyoyo zao zisipate kuikunjukia Imani, wasiamini mpaka waione adhabu kali iumizayo.» |