Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 84 - هُود - Page - Juz 12
﴿۞ وَإِلَىٰ مَدۡيَنَ أَخَاهُمۡ شُعَيۡبٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ وَلَا تَنقُصُواْ ٱلۡمِكۡيَالَ وَٱلۡمِيزَانَۖ إِنِّيٓ أَرَىٰكُم بِخَيۡرٖ وَإِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٖ مُّحِيطٖ ﴾
[هُود: 84]
﴿وإلى مدين أخاهم شعيبا قال ياقوم اعبدوا الله ما لكم من إله﴾ [هُود: 84]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tulimtuma kwenda kwa watu wa Madyan ndugu yao Shu'ayb, akasema , «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Nyinyi hamuna mungu yoyote anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, basi mtakasieni ibada.. Wala msiwapunguzie watu haki zao katika vipimo vyao na mizani zao. Mimi nawaona nyinyi muko kwenye ukunjufu wa maisha, na mimi nawachelea, kwa sababu ya kupunguza vipimo na mizani, adhabu ya siku itakayowazunguka |